Home > Random > Paruwanja wa Soap Operas

Paruwanja wa Soap Operas

Kuna mambo ambayo yanachukiza na kuleta raha kwa wakati mmoja, yaani, yanafurahisha watu wa kundi moja na vile vile kuwachukiza wengineo. Kwa mfano, mlo wa panya na konokono ni vitoweo vya kudhaminiwa na wanaoishi magharibi mwa Afrika mfano wa nchi ya Nigeria no mlo wa nyoka ni kitoweo wanachokienzi wachina lakini jaribu kufungua mkahawa wa kuuza vitoweo hivyo humu nchini Kenya. Hutapata wateja n’go! Pengine wachache ambao wangependa kuonja tu na pia itachukua muda mrefu kupata wafuasi wa kiwango cha kuwezesha biashara yako kunoga, au sivyo?

Kisa kama hicho cha panya, konokono na nyoka kimetupata kama wakenya. Utakubaliana nami, msomaji, kuwa filamu za mapenzi maarufu kama Soap Opera ambazo zimeshambulia vyumba vyetu vya mapumziko kupitia televisheni zetu kwa kuwa karibu runinga zote zinavyonyesha kila siku. Kinachasikitisha ni kuwa hata na malalamishi zinazochipuka kila mara, hakuna afueni tunapata na badala yake soap opera zinazidi kuongezwa kwa mipangilio wa programu.

Wanawake wengi ndio mashabiki wa vipindi hivi ingawa kuna wanaume kadhaa pia wanaotumbuizwa nazo. Hii imewafanya wanawake hao kujitetea kua wanaume hupenda sana kandanda na si vyema kuwa wao wanashurutishwa kuachana na soap opera na wanaume wenzao hawataki kuacha au kupunguza kuona michezo hayo ya kandanda ya ligi. Hata hivyo mimi binafsi si mfuasi wa mpira sasa nisipate kuangaliwa kijicho mithili ya viazi vilivyooza kwa kutoa maoni yangu hapa!

Ili kuwe na usawa wa kijinsia kama vile katiba inasema, basi vipindi vireje katika mpangilio wa hapo awali. Kuwe na mchanganyiko wa vipindi kutoka fani tofauti tofauti kama fiction, drama, vipindi vya humu nchini (na viwe vya dakika kama arobaini si vipindi fupi ambazo tunashuhudia siku hizi) na kadhalika bora tu tusizidi kuwekwa mateka na hizi soap opera.

Najua kuna msemo, kama huweziwashinda; ungana nao. Wenye runinga hizi ni wafanyibiashara na wangependa kuwa na watazamaji wengi na soap opera imekuwa kama sumaku kuwavuta watazamaji lakini wakae wakijua mbio za sakafuni si mbio za nyika ambozo watakimbia kushinda medali. Watu huboeka na kitu na tunavyojua wakenya hufurahishwa na kitu kwa muda mfupi kwa hivyo, waanze kushughulikia watazamaji wengine pia mapema.

Mikakati ya kuleta televisheni ya dijital ziko tayari na hiyo italeta afueni kwa kuwa natumai itakuwa rahisi kugawanyisha vipindi katika runinga tofauti kwa mfano, vipidi vya soaps vitagawiwa runinga yao n.k. afueni ilioje!

***

Stesheni za radio hazijasazwa. Hekaya zinazohusisha ngono ni tele si haba. Najua wenye kusimamia vipindi hizo wanasema “kama hupendezwi funga masikio” lakini haitawauma matumbo wakiweka vipindi hizo wakati ufaao kama usiku wakati watoto (na mimi) wamelala fofofo.

Ni hayo… au kiasi. Ingawa mie si mtaalamu wa lugha hii ya Kiswahili, nimefurahia kukitumia katika andiko hili. Pengine nitalitafsiri kwa lugha ya kimombo siku nyingine, kama bado hizi soap opera zitozidi kuwa kero!

Advertisements
Categories: Random
  1. January 30, 2012 at 4:34 pm

    Hata nimeshindwa kucomment! hehehe

  1. No trackbacks yet.

Thanks for your thoughts!

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: